February 1, 2016

KIIZA AKISHANGILIA NA AJIBU...

Hamisi Kiiza ameshaifungia Simba mabao 12 msimu huu lakini ameweka wazi kuwa hivi sasa shauku yake ni kuhakikisha timu yake hiyo inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Kiiza alisema katika mzunguko huu wa pili uliobakia, wanahitaji kujituma kwa nguvu zote ili kuweza kuisaidia timu hiyo kumaliza ligi katika nafasi nzuri na hata ikiwezekana kutwaa ubingwa.

“Mechi 14 zilizobakia kwenye ligi ni nyingi, hivyo tunahitaji kujituma ipasavyo kuweza kufanikiwa kushinda katika kila mechi, kuhakikisha tunafanikiwa kutwaa ubingwa kwani lengo langu ni kuona tunafikia malengo.


“Nipo Simba kwa ajili ya kuisaidia na sihitaji maneno mengi zaidi ya kujituma uwanjani na nitakuwa na furaha nikiona inafanikiwa kutwaa kombe,” alisema Kiiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic