WACHEZAJI WA COASTAL UNION WAKIWA PAMOJA NA MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI YA USAJILI YA COASTAL UNION, SALIM BAWAZIR WALIYEMLAZIMISHA KUPIGA NAYE PICHA. |
Mwisho wachezaji wa Coastal Union uvumilivu umewashinda kabisa na wameamua kuonyesha makali yao.
Wachezaji wa Coastal Union wanadai mshahara wa miezi mitatu pamoja na posho kadhaa ambazo hawajalipwa.
Baada ya kuvumilia kwa kipindi kirefu wameonekana kuchoshwa na hali hiyo, badala yake wamefikia uamuzi wa kumlazimisha mmoja wa viongozi walio katika kamati ya usajili, Salim Bawazir wapige naye picha wakiwa na bango lenye maneno haya “Coastal, wachezaji tunataka pesa zetu zote za mishahara.”
Taarifa zinaeleza wachezaji hao, nusura wamtandike kiongozi huyo alipotaka kugoma kupiga nao picha wakiwa na bango hilo.
Pamoja na kuonyesha uwezo kwa kuzishinda timu kama Yanga, Azam FC bado wachezaji hao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu sana.
Hali ambayo inaonekana kuwashinda na sasa wanachotaka ni kuona mambo yanafikia mwafaka kwa wao kulipa stahiki zao, au hawataichezea timu hiyo kuanzia katika michuano ya Kombe la Shirikisho na hata Ligi Kuu Bara kwa kuwa wamechoka kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment