February 19, 2016


Mashabiki wa Simba na Yanga wa jijini hapa, jioni ya leo Ijumaa watakuwa safarini kuelekea Dar kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa timu hizo unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Katibu Msaidizi wa Tawi la Yanga Mbeya, Lusajo Kifamba, amesema wapenzi na wanachama wa klabu yake pamoja na wale wa Simba, wamechangishana fedha shilingi 50,000 kila mmoja kwa ajili ya safari hiyo ambayo ni gharama za kwenda na kurudi.

Lengo la mashabiki hao kwenda Dar es Salaam kushuhudia live mechi inayozikutanisha timu zao kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo ni gumzo nchini, kwani atakayepoteza anaweza kupotea katika mbio za kuwania ubingwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic