February 22, 2016


“Ukicheza kwa kujiamini ni wazi utashinda.” Hiyo ni kauli ya Kocha wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm baada ya kuiongoza timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba, juzi Jumamosi.

Yanga na Simba zilipambana juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo kipigo kwa Simba kimekuja baada ya kucheza kwa takriban dakika 630, sawa na mechi saba bila ya kupoteza, sita zikiwa ni za ligi na moja ya Kombe la FA, Simba ikiwa inanolewa na Mganda, Jackson Mayanja.

Awali Pluijm aliifunga Simba ambayo ilikuwa imecheza kwa takriban dakika 270 sawa na mechi tatu bila ya kupoteza wakati huo ikiwa inafundishwa na Muingereza, Dylan Kerr.

Mchezo wa kwanza Yanga iliifunga Simba mabao 2-0, matokeo hayo yakajirudia tena juzi Jumamosi na kuifanya timu hiyo msimu huu kukusanya pointi zote sita mbele ya Simba.

“Siri kubwa ya kuibuka na ushindi katika mechi kama hii ni kujiamini na si kingine, wachezaji wangu wote walijiamini, ndiyo maana tukapata matokeo mazuri.

“Kila mmoja alicheza kwa nafasi yake, nampongeza Pato Ngonyani kwa kucheza vizuri leo (juzi), sikuwa na wasiwasi naye, ndiyo maana nilimpanga kwani kabla ya kumpa nafasi mchezaji huwa namchunguza uchezaji wake akiwa mazoezini na katika mechi za nyuma,” alisema Pluijm.


Kutokana na matokeo ya juzi na yale ya mechi ya mzunguko wa kwanza, ni dhahiri Pluijm amekuwa mwiba mchungu kwa makocha wa Simba msimu huu kutokana na kuwafunga wote, tena ikiwa ni baada ya kucheza mechi nyingi bila ya kufungwa.

1 COMMENTS:

  1. Football ni mchezo wa kusoma makosa ya mpanzani wako na ndio kinachomsaidia Pluijm,Kwa tabia ya ufundishaji wake nilijua Yanga wakirudi toka half time lazima wataongeza mabao.Hongera zao Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic