| NAPE |
Ishu ni kutumbuana majipu tu. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye jana Ijumaa amemfuta kazi Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Henry Lihaya.
Uamuzi huo wa kumfuta kazi Lihaya umekuja siku chache baada ya Nape kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo na naibu wake, Juliana Yasoda ambaye amehamia BMT.
Taarifa zinasema kuwa Nape amefikia uamuzi huo wa kumtoa Lihaya kutokana na kukaa kwenye wadhifa huo kwa muda mrefu bila kuonekana maendeleo ya kueleweka na amemteua Mohammed Kiganja kukaimu nafasi hiyo mpaka atakapoteuliwa katibu mpya.
Ofisa Habari wa BMT, Najaha Bakari, alisema wamepata taarifa hiyo ya waziri na utekelezaji wake umeanza jana hiyohiyo.
“Ni kweli Waziri Nape amemuondoa katibu (Lihaya) na kumpeleka wizarani, nafasi yake amekaimu Mohammed Kiganja mpaka pale mwenyekiti atakapompelekea majina matatu ya makatibu ambapo mmoja atateuliwa.
“Sababu ni kwamba katibu amekaa muda mrefu madarakani hivyo waziri anataka mtu mpya ili aendane na kasi ya sasa,” alisema Najaha.
Alipotafutwa Lihaya alisema: “Kwa sasa sina lolote la kusema.”







0 COMMENTS:
Post a Comment