February 9, 2016





Yanga inaondoka kesho kwenda nchini Mauritius tayari kuwavaa Cercle de Joachim SC.

Kikosi cha wachezaji 21 na viongozi 6 kinaondoka kesho alfajiri kwenda Mauritius  kwa ajili ya mechi itakayopigwa wikiendi.

Msemaji wa Yanga, Jerry Muro amesema tayari kila kitu kimekamilika kwa ajili ya safari hiyo kwenda kuanza kutupa karata ya kwanza ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Kila kitu kipo vizuri kabisa, leo timu imefanya maandalizi ya mwisho hapa nyumbani kabla ya safari hiyo kesho,” alisema Muro.

Katika mazoezi ya leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Yanga walifanya mazoezi ya nguvu ikionyesha Kocha Hans van der Pluijm anataka wawe fiti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic