Kazi imeanza na Yanga wanaonekana kuingia kwenye vita ya kuwakomesha wanaopenda "dezo".
Matapeli wengi hawapendi kufanya kazi na wanapenda vitu laini tu huku wakijua wengine wanahangaika.
Yanga wamepania kupambana nao na kukomesha hilo baada ya kuwanasa jumla ya washukiwa wanne ambao walikuwa wakitengeneza tiketi feki za mchezo wa leo dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius.
Yanga itakuwa uwanjani kesho kesho kuwavaa Cercle katika mchezo ya pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali, huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 ugenini wiki mbili zilizopita.
Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema katika oparesheni yao jana wamewakamata watu wanne maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam wakijaribu kucheza mchezo huo wa kitapeli na adui dhidi ya mali za klabu hiyo.
Amesema wanaendelea watu hao wako chini ya Jeshi la Polisi Tanzania ambalo limewashikiliwa wakiendelea kufanua uchunguzi kujua wahusika wakuu kabla ya ufikishwa kwenye vyombo vya dola.
Alisema kutokana na tukio hilo, mashabiki kuwa makini katika ununuaji wa tiketi.
Pia akasema hivi, jana walilazimika kusitisha baadhi ya vituo vya uuzaji wa tiketi hizo na kubakisha vituo viwili tu; klabuni na Karume wakati leo tiketi halisi zitakuwa zikipatikana kwenye Uwanja wa Taifa.
“Nianze kwa kutoa tahadhari kwa wadau wote kuwa makini, wajichunge na matapeli. Kuna watu mitaani wanatengeneza tiketi bandia, leo (jana) katika ucunguzi wetu tumewfanikuwa kukamata watu wanne, wengine walivyotuona wakakimbia. Watu hao tunawashikilia na tuaendelea kuchunguza kujua akina nani wako nyuma yao, kisha tutawafikisha polisi," alisema Muro.
0 COMMENTS:
Post a Comment