February 12, 2016

YONDANI

Kikao cha Kamati ya Kusimamia na Kuendesha ligi (Kamati ya Masaa 72) kimekutana Jumatano katikati ya wiki kupitia taarifa na ripoti mbalimbali za michezo ya Ligi Kuu (VPL), na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendeea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali nchini.

Ligi Kuu ya Vodacom
Mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000 (laki tano) baada ya kumpiga usoni kwa box la dawa Dk Mganga Kitambi wa Coastal Union wakati akitoa huduma kwa kipa wake katika mechi namba 121 kati ya timu hizo iliyofanyika Januari 30, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Yondani alitenda kosa hilo baada ya kumuomba maji Daktari huyo, lakini akamnyima. Adhabu huyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 ambapo baada ya kutumia adhabu ya mechi hizo, hataruhusiwa kucheza hadi atakapokuwa amelipa faini hiyo.

Naye Dk Kitambi anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kitendo chake cha kumrudishia Yondani kwa kumpiga ngumi. Kitendo cha Daktari huyo ni kinyume cha Kanuni ya 41(2), na pia Kanuni ya 36 kuhusu mchezo wa kiungwana.

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya Sh 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuwatupia chupa za maji wachezaji wa Coastal Union walipokuwa wakishangilia bao la pili.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic