March 26, 2016


Ukiachana na kukosa video za mechi za Yanga za hivi karibuni, Al Ahly inapambana kuhakikisha inakuwa vizuri kabla ya Aprili 9, mwaka huu itakapocheza na Wanajangwani hao.

Yanga itacheza na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kisha kurudiana wiki moja baadaye.

Mkurugenzi wa Michezo wa Al Ahly, Syed Abdul Hafiz, amesema timu yake imepata ugumu kuelekea mchezo huo baada ya kushindwa kupata video za Yanga katika mechi zake mbili za mwisho dhidi ya APR.

“Ubalozi wetu (wa Misri) nchini Tanzania umetuthibitishia kwamba mechi ya Yanga na APR haikuonyeshwa na televisheni yoyote ile, hivyo hatuwezi kupata video ya mechi hiyo.

“Sasa tunatafuta video ya mechi yao ya kwanza iliyochezwa Rwanda na tumemuagiza ofisa ubalozi wetu kule atupe hiyo video, tunachotaka ni video ya mechi za mwisho za Yanga,” alisema Hafiz.


Katika raundi ya kwanza ya ligi hiyo, Yanga iliitoa APR kwa mabao 3-2, kwanza ilishinda mabao 2-1 Kigali, Rwanda kisha ikatoka sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV