March 26, 2016

MKWASA BAADA YA KUTUA DAR NA KIKOSI CHAKE...
Kocha Taifa Stars, Charles Mkwasa, amesema baada ya kazi ngumu ya kuichapa Chad kwa bao 1-0 nchini kwao, kilichobaki ni kuifunga tena timu hiyo keshokutwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Katika mchezo wa kwanza wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 uliochezwa nchini Chad Jumatano iliyopita, Taifa Stars ilishinda bao 1-0 lililofungwa na nahodha Mbwana Samatta.

Mkwasa alisema hayo wakati akizungumza jijini Dar baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere usiku wa kuamkia jana Ijumaa akitokea Chad na kikosi chake. 

Akiwa uwanjani hapo, Mkwasa alisema; “Chad wapo vizuri hivyo hatuwezi kuwafanyia mzaha, tunachotakiwa ni kuongeza maarifa ili tuweze kuwafunga kirahisi tukiwa hapa nyumbani.”

Mkwasa alisema moja ya changamoto anazoweza kukutana nazo katika mechi ya marudiano Jumatatu ni majeruhi wawili, kiungo Mwinyi Kazimoto na beki wa kati Kelvin Yondani.


“Hii ni changamoto kuumia kwa Kazimoto na Yondani lakini hakuwezi kutuvurugia mipango yetu, kikosi chetu kipo vizuri kina wachezaji wa kutosha hivyo nawaomba Watanzania waje uwanjani kutuunga mkono,” alisema Mkwasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic