Kikosi cha wachezaji 24 wa Azam FC kinatarajia kuondoka nchini kesho kwa ajili ya mechi yake ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Bidvest.
Azam FC inakwenda nchini Afrika Kusini kwenda kuwavaa wenyeji wake hao ambao wanatokea katika jiji la Johannesburg.
Msemaji wa Azam FC, Jaffari Iddi ‘Mbunifu, amesema kila kitu kimekamilika na wako tayari.
“Tuko tayari na kila kitu kimeenda vizuri. Tunasubiri kesho safari ianze kwenda Afrika Kusini.
“Huko tutakuwa na siku kadhaa za maandalizi kabla ya Jumamosi ambayo itakuwa ni siku ya mechi,” alisema.
Bidvest ambayo inamilikiwa na moja ya chuo kikuu kikongwe nchini Afrika Kusini imekuwa ikiifuatilia Azam FC kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kurekodi mechi zake. Azam FC wanasema wanajua kila kitu kinachoendelea.
0 COMMENTS:
Post a Comment