JKT Ruvu ina pointi 21 na ipo katika hatari ya kushuka daraja katika Ligi Kuu Bara, baada ya kuona hali hiyo kocha wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni amewapa masharti wachezaji kuwa ni lazima washinde mechi saba zilizobaki.
Kibadeni nyota wa zamani wa Simba aliyewahi kuichezea na kuinoa timu hiyo, anataka timu yake ipate pointi 21 ambazo akichanganya na ilizonazo sasa atafikisha 42 ambazo zitawahakikishia kubaki ligi kuu.
Sasa JKT Ruvu ipo katika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 21 nyuma ya Toto Africans yenye pointi 23, ikifanya vibaya ina nafasi kubwa ya kushuka daraja.
Kibadeni amesema timu yake ipo katika nafasi mbaya hivyo wanahitaji kujikwamua kutoka katika nafasi hiyo kwa kuhakikisha wanajituma katika mechi zao za mwisho.
“Tupo kwenye nafasi mbaya sana tunahitaji kushinda kila mchezo kati mechi ya saba zilizobaki, tunaanza mchakato huo katika mechi dhidi ya African Sports.
“Nimewataka wachezaji kutumia muda huu wa mapumziko kidogo kuweza kujiandaa kwa kujituma ili kufanya vyema katika mechi zetu zote na kupata pointi tatu katika kila mchezo,” alisema Kibadeni.
0 COMMENTS:
Post a Comment