March 28, 2016


Na Saleh Ally
Picha hii kubwa ilipigwa Mei, 2013 wakati wachezaji haws watatu, Harry Kane, Jamie Vardy na Drinking Water wakiwa bench katika kikosi cha Leicester City.

Leo wachezaji hao ni tegemeo kwa Tottenham na Leicester zinazowania ubingwa wa England kwa karibu kabisa, pia ni tegemeo katika kikosi cha England.

Haikuwa rahisi, lazima walipambana vilivyo wakafanikiwa. Lazima walijua kuwa benchi kunahitaji juhudi za dhati kupata nafasi. Walijikubali, wakajitambua na kufanya kweli.

Wachezaji wengi wa hapa nyumbani, benchi wanaona ni sehemu kama adhabu, au kama si sahihi wanachukulia ni kama uonevu kwao.

Huenda picha hii inaweza ikawa funzo kwenu, kwamba kukaa benchi ni sehemu ya changamoto kufanya vema katika maisha yako ya soka.

Badala ya kuona unaonewa na kujimaliza kabisa, vizuri uone hiyo ni changamoto na unapaswa kuitumia vizuri kama sehemu ya kuinuka.

Vardy na wenzake wangeona wanaonewa, basi leo wasingekuwa na nafasi katika timu zao hadi kuitwa tegemeo.

Wako ambao wanamalizwa na maneno ya makundi, kukaa pamoja na kulalamika badala ya kutenda. Hii picha ni zawadi kwenu.

Maneno pekee bila ya juhudi na maarifa, hayawezi kuwa msaada wa mabadiliko kihatua kwa maana ya ubora kiutendaji.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic