March 8, 2016

KAZIMOTO

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangza kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini Dj'amena.

Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit katika mazoezi wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.

“Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa wikiendi ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katika timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo hautakuwepo.

"Ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa machi 23, 2016” alisema Mkwasa.

Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni makipa;
Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC).

Walinzi;
Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein 'Tshabalala' (Simba SC).

Viungo;
Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).

Washambuliaji;
Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Ajibu (Simba SC).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic