Mechi ya kuwania kucheza Afcon kati ya Nigeria waliokuwa wenyeji wa Misri kwenye Uwanja wa Ahmadu Bello mjini Kaduna iliisha kwa sare ya mabao 1-1.
Lakini utaona ilivyokuwa hatari kutokana na idadi ya watu kuzidi takribani mara mbili. Kwani Uwanja huo una uwezo wa kubeba watu 25,000 tu lakini walioingia walikuwa 40,000 na ushee.
Inaelezwa wengi walijitokeza kumuona kiungo wa Arsenal, Iwobi aliyegoma kuichezea timu ya taifa ya England na kurejea nchi yake ya asili na kuichezea Nigeria.
Ukiangalia mazingira ya Uwanja wa Ahmadu Bello, hakika ni yaliyochoka. Huwezi kulinganisha na viwnaja vyetu hasa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Bora kuipenda Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment