March 23, 2016




Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na msemaji wa klabu ya Simba, leo amewasilisha barua yenye malamiko ya klabu hiyo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), pia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Barua hiyo ya Simba kwenda kwa TFF na kopi kwa Nape, inawalalamikia pia wachezaji wawili nyota wa Yanga, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kutokana na vitendo vyao vya nidhamu huku shirikisho hilo lilionekana kuvifumbia macho.

Pamoja na hivyo, sehemu ya barua hiyo, inaeleza Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro kutumia lugha za kibaguzi pamoja na kuonyesha dharau kwa kutoa kauli ambazo si za kiungwana.

Simba inawatuhumu Tambwe kwa kumvuta korodani Juuko Murshid na Ngoma kumpiga kichwa kwa makusudi beki Hassan Kessy lakini kamati ya nidhamu chini ya TFF, kamwe haijawahi kukaa na kusikiliza, badala yake inaonekana kuziba masikio.

Manara alikabidhisha barua hiyo TFF mbele ya waandishi wa habari ili kuonyesha kuwa kweli suala hilo limefika. Lakini akafanya hivyo pia kwa Waziri Nape.

Pia barua hiyo ya Simba iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Amos Gahumeni, imetaka TFF kuhakikisha Azam FC, Yanga nazo zinacheza mechi zake mbili za viporo ili kuepusha suala la upangaji matokeo mwishoni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic