Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga dhidi ya Azam FC ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2, Jumapili.
Lakini gumzo kubwa kwa wadau wa soka mtandaoni ni namna beki Vicent Bossou alivyokuwa akiteseka kila alipojaribu kuwazuia Kipre Tchetche na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Bossou raia wa Togo alionekana ni mzito kuwazuia viungo hao ambao ni wepesi na wana kasi.
Mashabiki wa soka katika mitandao mbalimbali wamekuwa wakimjadili Bossou namna alivyoteseka huku wakitupia picha mbalimbali zinazoonyesha alivyokuwa akinyanyaswa.
0 COMMENTS:
Post a Comment