March 30, 2016



Kocha Jackson Mayanja wa Simba amesema kila mchezaji lazima akumbuke, nidhamu linaweza kuwa suala la kujivunia milele na akatoa mfano wa marehemu Abel Dhaira.

Mayanja amesema kila mchezaji au mdau wa soka la Uganda, kila anapozungumza kwa sasa anazungumzia suala la nidhamu.

“Ukimzungumzia Dhaira kwa sasa hauwezi kutotaja suala la nidhamu, leo hatunaye leo ni majonzi makubwa lakini tunaendelea kumkumbuka kwa suala la nidhamu.

“Mwenyezi Mungu ampumzishe lakini ataendelea kuwa na sifa ya utendaji bora pamoja na suala la nidhamu,” alisema Mayanja.


Dhaira aliyewahi kuwa kipa wa Simba, amefariki dunia wiki iliyopita baada ya kubainika anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo.

2 COMMENTS:

  1. Mmmh!marehemu siku zote wanakuwa wazuri.R.I.P Dhaira.

    ReplyDelete
  2. Mayanja anasikika kwenye vyombo vya habari kuliko
    waziri,TFF.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic