March 21, 2016Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amesema anakiamini kikosi chake na kutamka kuwa yupo tayari kuivaa Al Ahly ya Misri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga ambayo iliitoa APR katika raundi ya kwanza, imetinga raundi ya pili na itakutana na Al Ahly Aprili 9 jijini Dar kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye. Al Alhy yenyewe iliifungashia virago Recreativo do Libolo ya Angola.

Pluijm amefunguka kwa kusema kuwa anaijua vizuri Al Ahly kutokana na kuwahi kukutana nayo mara kadhaa katika michuano hiyo hata kabla hajatua Yanga. Pluijm aliwahi kuifunga Al Ahly bao 1-0 mwaka 2014 jijini Dar lakini timu yake baadaye ilitolewa kwenye michuano hiyo kwa mikwaju ya penalti.

Aidha kocha huyo makini alieleza kuwa iwapo atakutana na timu hiyo mchezo utakuwa mgumu na wa kiushindani lakini dakika 180 ndizo zitakazoamua  kwa kuwa ana kikosi kizuri.

“Siihofii Al Ahly ni timu nzuri na yenye ushindani lakini siwezi kusema kuwa nitaifunga. Naijua vizuri Al Ahly kwani nimeshawahi kukutana nayo nikiwa hapa Yanga na kabla ya kutua hapa, kinachotakiwa ni kujiandaa kukabiliana na mechi hiyo kwani nina kikosi kizuri cha kiushindani,” alisema Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV