March 2, 2016


Ruvu Shooting Inatarajia kumuongeza mkataba mwingine kiungo wake Shabani Kisiga, hii ni baada ya ule wa awali kufikia kwisha.

Kisiga alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliyoirejesha Ligi Kuu Bara, Ruvu Shooting akiwa na wakongwe wenzie ambapo mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo umeisha.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema bado wanamuhitaji Kisiga kuendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu na kudai kuwa kwa sasa wapo katika mazungumzo naye.

“Tulikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Kisiga ambao umefikia tamati mwishoni mwa msimu huu, hivyo ni miongoni mwa wachezaji tunaowahitaji kwa ajili ya kuitumikia timu yetu msimu ujao.

“Tunatarajia kumuongeza mkataba mwingine kwa ajili ya kuitumikia timu yetu msimu ujao kwani kiwango chake ni kuzuri na tungependa kuendelea naye katika msimu ujao.

“Tuna mikakati ya kuongeza wachezaji katika usajili unaokuja ili kuweza kupata vijana watakaosaidia kuongezea nguvu kikosi chetu,” alisema Bwire.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic