March 2, 2016



Kufuatia Coastal Union ya Tanga kuwa kwenye migogoro kwa sasa huku ikiwa kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, kocha wa timu hiyo, Ally Jangalu ameibuka na kusema kuwa migogoro hiyo wao wala haiwahusu na wanapambana kuinusuru timu hiyo.

Coastal ambayo imetinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kwa sasa ipo kwenye nafasi ya tatu kutoka mkiani kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 16, hivyo inahitaji kufanya kazi ya ziada kujitoa kwenye nafasi hiyo ili mwisho wa msimu isishuke daraja.

Jangalu amesema yeye na wachezaji wake mambo ya viongozi huwa hawajihusisishi nayo, hivyo haitawaharibia mipango yao ya kujitoa kwenye hatari ya kushuka daraja.
“Sisi kazi yetu ni kucheza mpira na ndicho kilichotuleta Coastal hivyo mambo mengine ya uongozi huwa tunajiweka nayo kando.


“Tutapigana kwa kadiri tuwezavyo mpaja tuione Coastal inapata mafanikio, nitawajenga kisaikolojia wachezaji wangu ambapo itawasaidia kupata nguvu ya kupambana kwa kusaka ushindi katika mechi zote zilizobaki,” alisema Jangalu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic