April 16, 2016

KULIA NI MENEJA WA AL AHLY YA MISRI AMBAYE ALIWAHI PIA KUJA NCHINI KABLA TIMU YAKE HAIJAPAMBANA NA YANGA. SASA WA TIMU YA TAIFA NAYE TAYARI YUKO NCHINI...

Wababe wa soka Afrika Misri, kweli wamepania kufuzu fainali za Kombe la Afrika 2017 (Afcon), kwani tayari meneja wa timu hiyo ametua nchini kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kabla ya mechi yao dhidi ya Taifa Stars.

Timu hizo, zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa Kundi G la michuano hiyo Juni 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Misri wataivaa Stars wakitoka kuifunga Nigeria bao 1-0, baada ya awali kutoka sare ya bao 1-1 nchini Nigeria. 

Taarifa za uhakika zinasema meneja wa timu hiyo, Ihab Leheta yupo nchini kwa ajili ya kuandaa mazingira ya mchezo huo.

“Meneja wa Misri yupo nchini tangu Jumatano iliyopita na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) wanazo taarifa za ujio wake, huyu amekuja kuandaa mazingira ya timu itakapofikia na mambo mengine.

“Inavyoonekana wamepania kufuzu fainali hizi na ndiyo maana wameonekana kuanza maandalizi ya mchezo huo ikiwa ni miezi miwili kabla,” alisema mtoa taarifa huyo.

Katika michuano hiyo ya kufuzu, Stars ipo Kundi G ikiwa na timu za Misri, Nigeria huku Chad wakijitoa. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV