April 22, 2016Kikosi cha Azam FC kimewasili jiji Dar es Salaam, leo mchana kikitokea nchini Tunisia ambapo huko kilicheza dhidi ya Esperance de Tunis na kutolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Mara baada ya kuwasjili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, kikosi hicho cha Azam FC kilienda katika hoteli ya jirani na uwanjani hapo kwa ajili ya mapumziko mafupi kisha baadaye jioni ya leo kuanza safari ya kuelekea Mwanza.

Azam itaelekea Mwanza ikiwa ni katika kujiandaa na mechi dhidi ya Mwadui FC katika Kombe la FA, machezo ambao unatarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumapili.


Azam ilitolewa katika michuano hiyo ya kimataifa kwa jumla ya mabao 4-2, kwa kuwa licha ya kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kwenye mchezo wa marudio wa Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho.
Mara baada ya kutua Mwanza timu hiyo itapumzika kabla ya kuelekea Shinyanga ambapo huko ndipo itakapocheza mchezo huo wa nusu fainali dhidi ya timu ambayo inanolewa na Kocha Jamhuri Kiwelo ‘Julio’.


PICHA: AZAM FC

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV