April 22, 2016Kikosi cha Simba kimeondoka leo mchana jijini Dar es Salaam kuelekea Unguja kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Mei Mosi mwaka huu.

Simba inayonolewa na Mganda, Jackson Mayanja, kwa kipindi kirefu imekuwa na desturi ya kwenda Unguja pindi inapokabiliwa na michezo migumu hasa dhidi ya Yanga. 

Meneja wa Simba, Abbas Ally amesema kuwa kikosi hicho kinaenda ‘camp’ hiyo kikiwa na lengo la kwenda kusaka muarobaini wa kuchukua pointi tatu watapokutana na Azam.

Kwa uamuzi huo inaonyesha kuwa mechi huo pia wameuchukulia kwa uzito na inaonyesha kuwa kweli wanahitaji ushindi hasa kutokana na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Toto Africans kwenye Uwanja wa Taifa, Jumapili iliyopita.Simba  inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 57 nyuma ya Yanga yenye pointi 59, Azam ikiwa nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi 55 lakini Yanga na Azam zipo nyuma kwa mchezo mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV