April 22, 2016Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas ametoa kauli ambayo inaonekana ni tata kuhusu kipindi cha wakati mgumu ambacho timu hiyo ilikuwa ikipitia chini ya Kocha Jose Mourinho.

Fabregas amesema kuwa ilifikia kipindi akawa anahisi amesahau kucheza soka na alikuwa akiingia uwanjani lakini hajui anachokifanya akiwa ndani ya uwanja kutokana na timu yake kuwa na matokeo mabovu.Kiungo huo ni mmoja wa wachezaji waliokuwa wakitajwa kucheza chini ya kiwango na kusababisha Mourinho kufukuzwa kazi kutokana na matokeo mabaya licha ya kuwa wao ndiyo waliokuwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’.

“Kuna wakati baada ya mechi dhidi ya Bournemouth nilikuwa nimelala kitandani, nilikuwa na masikitiko sana na kilichokuwa kikiendelea klabuni, nikamwambia mke wangu kuwa nimesahau hata jinsi ya kucheza mpira,” alisema Fabregas alipokuwa akizungumzia suala hilo kisha akaendelea:

"Sikuwa mimi, nilikuwa niponipo tu, ilifikia hatua ninampira lakini sijui niufanyie nini na sijui nimpasie nani.

"Hiyo miezi miwili au mitatu nilipoteza kabisa hali ya kujiamini.”


  Baada ya kuondoka kwa Mourinho kutokana na matokeo mabaya, angalau Chelsea ilianza kupata nafuu ya kupata matokeo ikiwa chini ya kocha wa muda Guus Hiddink tangu Desemba, mwaka jana.

"Nashukuru Mungu kila kitu kilienda vizuri na kubadilika na nikawa nacheza vizuri."

Licha ya matokeo mazuri kiasi bado mwendo wa timu hiyo haikuwa bora kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo mpaka sasa inashika nafasi ya 10 katika msimamo wa Premier League.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV