April 26, 2016


Manchester City ikicheza bila ya kiungo wake wa "mipango" Yaya Toure, imeshindwa kuifunga Real Madrid katika mechi kali ya Ligi ya Mabingwa iliyochezwa kwenye Dimba la Etihad na kumalizika kwa sare ya 0-0.

Pamoja na Madrid kumkosa Cristiano Ronaldo aliyekuwa jukwaani, lakini iliweza kutawala zaidi na kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.

Mechi hiyo ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilikuwa ni ya kuvutia na kila timu ilicheza kwa kujituma huku Sergio Aguero kwa upande wa Man City na Gareth Bale kwa upande wa Madrid wakionekana kuwa tatizo.

Kinda Kevin De Bruyne alizidi kuonyesha ni kati ya wachezaji hatari kabisa. Hata hivyo mabeki Sergio Ramos na Pepe waliweza kumthibiti.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV