April 4, 2016

Dk Sulaiman
Mmoja wa mabilionea wa Kiarabu, Dr Sulaiman Abdul Kareem Mohammed Al Fahim, sasa ndiye Mwenyekiti mpya wa klabu ya African Lyon.

Kutua kwake na uzoefu alionao katika soka kimataifa, unatafsiriwa kuwa ushindani mpya kwa Yanga, Simba na Azam FC.

African Lyon iliyowahi kumilikiwa na bilionea wa Kitanzania, Mohammed Dewji kabla ya kununuliwa mfanyabiashara Mtanzania mwingine, Rahim Zamunda, imerejea Ligi Kuu Bara msimu huu.

Al Fahim anaanza kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kuanzia Aprili 16 na atafanya kazi ya kuiinua na kuiboresha klabu hiyo kuwa moja ya timu bora na zenye ushindani katika Ligi Kuu Bara.


Kupitia Faheem Group, mona ya makampuni makubwa anayoyamiliki kutoka Abu Dhabi, Dk Sulaiman ambaye ni mzoefu na mambo ya soka la kimataifa, pia atawasaidia vijana kupiga hatua kisoka.

Taarifa zinasema bilionea huyo ana urafiki wa karibu na Sheikh Mansour bin Zayed Al Nahyan wa Abu Dhabi ambaye ni mmilikiw klabu ya Manchester City.
Akizungumza na SALEHJEMBE, mmiliki wa African Lyon, Zamunda amesema anamkaribisha Dk Sulaiman kwa mikono miwili.


“Imekuwa ni kama miaka mitatu au minne tokea tuanze kumshawishi Dh Sulaiman kuungana nasi. Lakini sasa tuna furaha kubwa kumkaribisha, pia tuna matumaini kwamba tutaweza kwenda vizuri na kujua ujio wa maisha ya baadaye ya klabu hii kwa uhakika, hii ni kutokana na uzoefu mkubwa wa soka kimataifa alionao,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV