April 4, 2016

NAPE AKIWA NA MKUU WA MKOA WA MBEYA, AMOS MAKALLA (KUSHOTO) KWENYE UWANJA WA SOKOINE MJINI MBEYA.

Mashabiki na viongozi wa Coastal Union wameonekana kutofurahishwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye kutinga jezi ya Mbeya City.

Nape alivaa jezi hiyo wikiendi wakati Mbeya City ‘ilipoitumbua’ Coastal Union kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Mashabiki hao walionekana wakipinga kwenye vyombo mbalimbali vya habari na mitandaoni wakiamini haikuwa sawa.

Lakini pia walikuwa wakilalamika kuhusiana na suala hilo, wakidai kwamba wanataka kumuona pia akiwa amevaa jezi ya Coastal Union.

Hata hivyo, baadhi hasa mitandaoni nao wamekuwa wakipinga na kuamini hakuna jipya katika hilo na Nape anaweza kuvaa jezi yoyote anayotaka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV