April 11, 2016


HUMUD...
Abdulharim Humud, ambaye alikuwa nahodha katika mechi ya leo wakati Coastal ikiangusha Simba katika mechi ya Kombe la FA, amesema watapambana kubaki Ligi Kuu Bara.

Humud ameyasema hayo mara tu baada ya kuiangusha Simba.

“Tumekuwa tukipambana sana, wakati fulani huwa kuna mambo magumu sana. Lakini utaona tulivyopambana hadi mwisho na kuwatoa Simba.

“Sasa tunataka kuhakikisha tunapambana hivi katika mechi zetu nne zilizobaki ili kubaki kwenye Ligi Kuu Bara,” alisema Humud.


Coastal ni kati ya timu zinazoburuza mkia katika Ligi Kuu Bara na zinaonekana ni nadra kukwepa kuteremka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV