April 11, 2016


MPIRA UMEKWISHA
- Kapama analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha akidanganya ameumia
DAKIKA 4+ ZA NYONGEZA
Dk 88 na 89, Simba hawaonyeshi matumaini yoyote ya kwenda kusawazisha
KADI Dk 87, Nimubona analambwa kadi ya njano kwa kumvuta jezi Mahadhi
Dk 86, Kiiza anapoteza nafasi baada ya shuti lake kutoka nje sentimeta chache


GOOOOOOOOOOO Dk 85 Sabo anaifunga penalti safi kabisa akimtesa kipa Agbani
Dk 83 PENAAAAATTT, Lufunga anamwangusha Shiboli na mwamuzi anatoa penalti kwa Coastal na kumpa kadi nyekundu Lufunga. Mabeki wa Simba walijichanganya, Shiboli akawazidi ujanja na kuingia neo la hatari

Dk 81, Kiiza anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga, mpira unaokolewa na mabeki KADI Dk 79 Humud analambwa kadi ya njano kwa kumpiga 'pepsi' Kessy, lakini anamlaumu mwamuzi Mahagi kwa nguvu zote
Dk 70 shuti Kiongera linazuiwa, mpira unamkuta Kiiza katika nafasi nzuri. Lakini Kiiza anapiga shuti kuuuubwaaaa
Dk 68, Angani anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Juma na kuwa kona, lakini inakuwa madhara kwa Simba
Dk 67, Mkude anawahadaa mabeki wawili wa Coastal lakini anapiga shuti 'mtoto' na Fikirini anadaka kwa ulainiii
SUB Dk 66, Simba inafanya mabadiliko ya mwisho kwa kumuingiza Rafael Kiongera kuchukua nafasi ya Lyanga
KADI 63, Adeyum analambwa kadi ya njano kwa kumzonga mwamuzi msaidizi

Dk 60, Kiiza anaruka na kupiga kichwa krosi ya Tshabalala lakini anashindwa kuupiga vizuri mabeki Coastal wanaokoa
Dk 58, Awadhi Juma anapiga shuti kali kimo cha kuku, mpira unagonga mwamba na kurejea uwanjani, mabeki Coastal wanaokoa
Dk 54, kona nyingine kwa Simba, Tshabalala anaimimina lakini vizuri kabisa lakini Coastal wanaokoa vizuri kabisa mabeki wa Coastal
Dk 53, Simba inapata kona baada ya Juma kuutoa mpira, lakini inakuwa haina madhara kwa Coastal
SUB Dk 52, Ahmed Ali Shiboli anaingia kuchukua nafasi ya Jailan

GOOOOOOO Dk 49, Kiiza anaifungia Simba bao la kichwa akiunganisha krosi nzuri ya Ajib
SUB Dk 47, Simba wanamtoa Majabvi anaingia Hamisi Kiiza
SUB DK 46, Simba wanamtoa Ndemla nafasi yake inachukuliwa na Awadhi Juma

MAPUMZIKO
-Ajib anaingia vizuri lakini Hamad Juma analala na kuokoa, kona. Simba wanaichonga lakini haina manufaa
-Daktari wa Coastal Mganga Kitambi anaingia kumtibu Mahadhi ambaye alikuwa chini baada ya kuanguka mwenyewe
-Mkude anaonekana ni kucheza vema zaidi na kuipandisha timu lakini hata hivyo mbinu za mwisho kwa washambuliaji wa Simba zinaonekana hazina msaada

DAKIKA 1+ YA NYONGEZA
Dk 44 Bado Simba hawaonyeshi mipango 'imarishi' kwamba ni watu wanaoweza kufunga bao katika kipindi hiki cha kwanza

Dk 43 Majabvi anapiga shuti kali kabisa mpira wa adhabu ndogo, lakini unatoka pembeni kidogo mwa lango la Coastal
Dk 41, Simba wanafanya shambulizi jingine zuri kabisa, lakini kinachoonekana ni kukosa utulivu katika suala la umaliziaji
Dk 38, Kipa Agbani wa Simba anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi wa Said Jeilan na mabeki wa Simba wanaokoa

Dk 36 Kessy anamtoka beki wa Coastal, akiwa pembeni ya uwanja, anajaribu kufunga na mpira unatoka nje, goal kick
Dk 35, Ndemla anapiga shuti kali kabisa lakini mpira unapita juu kidogo ya lango la Coastal Union
Dk 34, Fikirini anaonyesha umahiri tena kwa kuokoa mpira uliokuwa unajaa wavuni
DK 33, Kipa Bakari Fikirini anafanya kazi nzuri kabisa kudaka krosi nzuri ya Tshabalala baada ya Simba kugongeana

Dk 29, Kessy anaruka na kufunga baada ya shuti kali la Mkude, lakini mwamuzi msaidizi anasema alikuwa ameishaotea kabla ya kufunga mpira huo uliogonga mwamba

SUB Dk 31, Twaha Ibrahim 'Messi' anakwenda benchi na nafasi yake inashukuliwa na Nassor Kapama
Dk 30, Tshabalala anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa krosi wa Mahadhi na kuwa kona

Dk 29, mpira wa krosi unagongwa beki na kutoka nje, kona. Simba wanaochonga lakini haina manufaa kwao
Dk 22, Emiry Nimubona anawatoka mabeki wa Coastal na kupiga krosi safi lakini Ajib anachelewa
Dk 20, Ajib anaitoka difensi ya Coastal lakini kipa anatoka na kuuwahi mpira
Dk 19 GOOOOOOOO Sabo anapiga mpira safi wa adhabu na unekwenda moja kwa moja wavuni, Coastal inatangulia kwa bao moja

Dk 16 hadi 18, kinaonekana kudhibiri zaidi mpira zaidi na Coastal hawajipangi vizuri
Dk 15, Mahadhi anapata nafasi nzuri lakini kasi yake inafanya asiufikie mpira baada ya kipa na beki wa Simba kujichanganya
Dk 13 Simba wanafanya shambulizi zuri kwanza, krosi ya Nimubona inampita kipa wa Coastal, unamkuta Ajib lakini anafanya madudu tena
DK 10, mpira unaendelea, lakini bado unaonekana kupoa sana, hakuna timu iliyofanya mashambulizi makali
Dk 7 hadi 9, kipa wa Coastal anaonekana kupata 'hitilafu', anatibiwa


KIKOSI CHA SIMBA

Dk 6, Ajib anapata nafasi nzuri kabisa, lakini anapiga shuti dhaifu kabisa
Dk 5, Coastal wanapata kona ya kwanza, hata hivyo inakuwa haina madhara
Mechi imeanza na kila upande unaonekana kucheza kwa umakini mkubwa. Hata sasa hakuna shambulizi kubwa.


KIKOSI CHA COASTAL UNION

1 COMMENTS:

  1. Duh!
    wamatopeni walijiaminisha sana,wapi MAYANJA?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV