April 6, 2016



Kocha wa JKT Ruvu, Abdallah Kibadeni, ameweka wazi kuwa licha ya kuwa kwenye timu ndogo lakini anapata presha kubwa na hii yote kutokana na timu hiyo kuwa chini ya viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Kibadeni ambaye pia ni mshauri wa benchi la ufundi la timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, aliichukua JKT Ruvu mwanzoni-mwanzoni mwa msimu huu kutoka kwa Fred Felix Minziro, aliyeachia ngazi kutokana na matokeo mabaya aliyokuwa akiyapata.

Kibadeni alisema kuwa kinachotia presha ni pale ukifikiria kuwa umepewa dhamana kubwa na wakuu wa jeshi la kuiokoa timu yao huku ukipiga hesabu unaona timu inazidi kuwa kwenye nafasi mbaya.

“Sitaki kuiharibu timu yao ndiyo maana napambana kuhakikisha nafanya kila niwezalo timu inabaki kwenye ligi kuu msimu ujao.


“Unajua timu inamilikiwa na wanajeshi shughuli zote za timu tunafanyia kambini kwao kama ukifanya vibaya  lazima ujishtukie, kukutana na watu wenye vyeo halafu timu yao unaipeleka pabaya si mchezo lazima upate presha,” alisema Kibadeni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic