April 5, 2016

CHACHA
Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF kuanzia leo tarehe 5 Aprili 2016.

Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha alieleza kuwa amepata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia
yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho

Martin alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Afisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).


TFF inamtakia kila la kheri na mafanikio mema Chacha katika majukumu yake mapya.

Wakati Chacha anajiuzulu, yuko katika tuhuma kwamba anahusika kupanga matokeo baada ya sauti yake kusikika akipanga mambo na viongozi wa Geita Gold Mine.

Taarifa za sauti yake hiyo zimesambaa kwa nguvu katika mitandao mbalimbali nchini.2 COMMENTS:

  1. Kama ni sauti yake kweli basi huyo ni jipu,hatakiwi na hafai kuachwa kwenda kwenye kazi mpya.Huyo ni wa kutumbuliwa.

    ReplyDelete
  2. Kiongozi mzuri atapimwa kutokana na watu wanaomzunguka au watu anaowateua katika nafasi mbalimbali kwenye Taasisi anayoiongoza.Kwa sasa inatosha kwa Malinzi kuwaambia watu wake muda wa kuendelea kufanya kazi nao umepita kama fadhila amekwishawalipa aanze upya kurudisha heshima ya TFF aliyoachiwa na Tenga.Hali ya TFF kwa sasa inasikitisha huku madeni ya TRA,kule madeni ya mshahara ya kocha wa timu ya Taifa,huku kashfa za kupanga matokeo,huku ratiba mbovu ya ligi kuu n.k.Hivi ni viashiria tosha vya taasisi kuyumba hivyo lazima maamuzi magumu yafanyike kwa maslahi ya soka la Tanzania kwani TFF siyo taasisi ya mtu binafsi na kikundi cha marafiki aau ndugu.Nchi hii ina watu zaidi ya milioni 40 hatuwezi kukosa watu 10 wa kuongoza TFF kwa kiwango tunachokitaka ili kuleta mafanikio yanayokusudiwa.Uongozi ni ule uwezo wa kuweza kutumia vipaji vilivyopo ili kutimiza malengo ya taasisi

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV