KIKOSI CHA YANGA |
Yanga imetuma kiongozi wake mmoja mjini Cairo, Misri kuhakikisha anaweka mambo kabla ya kikosi hicho kuondoka nchini kesho.
Taarifa za uhakika zinaeleza kiongozi huyo wa Yanga, sasa ana siku ya nne akiendelea kufanya maandalizi kabla ya kikosi chake kutua Cairo.
“Kweli kuna kiongozi wa Yanga yuko hapa Cairo (anakataa kumtaja jina), na amekuwa akipata msaada mkubwa kuhakikisha maandalizi ya kuipokea timu yanafanyika vizuri,” kilieleza chanzo.
Yanga inakwenda Misri kuivaa Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 mjini Dar es Salaam.
Waarabu wamekuwa na mtindo huo na Yanga inaonekana kulitilia maanani suala hilo.
Mwaka juzi pia ilifanya hivyo kwa kumtuma aliyekuwa Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa kwenda kuisoma Ahly. Mwisho Yanga ilitolewa kwa penalti lakini yenyewe ikiwa “imeshindwa”.
0 COMMENTS:
Post a Comment