April 6, 2016


Baada ya Azam FC kushindwa kuondoka na pointi tatu kwenye mchezo wake wa kiporo dhidi ya Toto African ya Mwanza, kocha wa timu hiyo, Muingereza, Stewart Hall ameeleza kilichowaangusha siku hiyo kuwa ni uwanja na waamuzi wa mchezo huo.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza matokeo yalikuwa ni sare ya 1-1 yaliyoifanya Azam kuendelea kuwa wa tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 51 chini ya Yanga wenye 53  na Simba yenye 57.

Stewart amesema wachezaji wake walipambana mwanzo mwisho lakini ukiachilia mbali mechi yao na Toto, walilazimika pia kupambana na uwanja huo mbovu uliokuwa kikwazo kikubwa kwao. Kingine ni waamuzi wa mechi hiyo aliyodai walikuwa wakiwadidimiza.

“Vijana walijituma sana lakini tulikwamishwa na vita nyingine nje ya mechi ya Toto siku hiyo, tulilazimika kupambana na uwanja mbovu, ulikuwa umejaa maji na hatukustahili kuendelea kuutumia lakini pia waamuzi walitukandamiza kwa maamuzi yao.


“Kwa hiyo tulikuwa na vita tatu kwa wakati mmoja na mwisho mechi ikaisha kwa 1-1. Haikuwa mipango yetu kupata pointi moja, lakini sasa itatulazimu kupambana na kupata pointi zote sita zilizobaki kwenye viporo vyetu vya Ndanda na Mtibwa Sugar,” alisema Stewart.

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. Kwani hao TOTO wao waligeuka samaki hapo uwanjani hadi kuweza kucheza vizuri?Huyo kocha ameshaishiwa maarifa na kila timu zimeshaua mfumo wake,asubiri kutimuliwa atakapofungwa na wekundu wa msimbazi tuu

    ReplyDelete
  2. Hukosi sababu?una tabia mbaya siku hizi.
    msimu ukiisha ndio mwisho wako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic