April 29, 2016

HALL (KUSHOTO) AKIWA NA KOCHA MKUU WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM

Kocha Stewart Hall wa Azam FC ‘amenunua’ ugomvi wa Yanga na Coastal Union kwa kusema kuwa kuna kila sababu ya kujifikiria mara mbili kwa nini kila siku itajwe Yanga katika matokeo tatanishi na kuongeza kuwa Yanga haikupata ushindi halali kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho.

Mchezo wa Yanga na Coastal ulivunjika katika dakika 15 za mwisho za nyongeza ambapo Yanga ilikuwa ikiongoza mabao 2-1, baada ya kupitia ripoti ya mchezo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likaipa Yanga ushindi kwa madai kuwa mashabiki wa Coastal walikuwa chanzo cha mchezo huo kuvunjika.

“Kila mtu, kila kona hapa gumzo ni mchezo huo wa Coastal na Yanga, hata katika mitandao ya kijamii na Youtube yanayozungumzwa sana kuhusu soka la Tanzania ni hujuma, limejaa viashiria vya rushwa,” alisema Hall na kuongeza:

“Niliona mchezo ule, bila kificho mabao yote hayakuwa halali, bao la kwanza aliotea (Donald Ngoma), bao la pili wazi kabisa lilikuwa la mkono, lakini mwamuzi hakuwa na maamuzi. TFF wanatakiwa kufunguliwa mashtaka.

“Nimekuwa hapa mwaka wa sita sasa, soka linatawaliwa na rushwa lakini kwa sasa imezidi kiwango.”

Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) ipo kwenye uchunguzi wa kina kwenye soka kubaini mianya ya rushwa ambacho kimekuwa kilio cha Watanzania kila kukicha. 


SOURCE: CHAMPIONI

7 COMMENTS:

  1. Sitegemei Hall aisifie Yanga kwakuwa hana tofauti na wewe!! Mangapi yanafanyika kwenye EPL je ni rushwa!? Kama anajua kuna rushwa basi alete ushahidi, watu kama hawa kwenye ligi zilizoendelea huwa wanafungiwa. Timu ina kila kitu kiuanzia pesa, uwanja mpaka wachezaji wazuri lakini bado inaboronga kwenye international game. Anadhani anaweza kujificha kwenye kivuli cha Yanga!? Hatutaki siasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo Hall huu ndio msimu wake wa mwisho kuwa Azam,tumemvumilia tumechoka hakuna maendeleo ya soka Azam bora tubaki na akina Dennis kitambi tuu

      Delete
  2. Wewe umezidi sasa ujawai ona epl magoli yanafungwa hivyo so timu za epl zinatoaga rushwa nazo au... umekosa habari za kuandika

    ReplyDelete
  3. Azam wanende hatua moja mbele. Huyu Hall alikwepo wakamtimua, baadaye amerudi tena. Wamekosa makocha wengine dunia nzima ni Hall tu. Kama anajua mpira wa Tanzania umejaa rushwa, si aende sehemu hakuna mambo hayo? Hapa Tanzania anatafuta kitu gani?

    Anajua mshindani wake ni Yanga tu. Hayo maneno ni utetezi in case wakifungwa na Simba Jumapili.

    ReplyDelete
  4. Kuna kitu sikielewi kwa watanzania hasa huyu Saleh Ali mwandishi kwanza hao Azam TV Wameshindwa kabisa kuthibitisha kwamba Ngoma alikua offside kwani camera zao zinaonyesha mchezaji wa coats union beki anakimbia nafasi yake kurudi mbele kuua offiside trick hilo media hamsemi angalieni vizuri au waambie azam tv warudie hayo matukio mawili kwa umakini. pia goli la Tambwe azam tv imeshindwa kuonyesha na kuthibitisha bila chenga kwamba Tambwe alifunga kwa mkono. sasa kwa kuzingatia hayo hapo juu unawezaje kuhukumu ww saleh na huyo stuart wako. juzi uliandika a very stupid article kamamwandishi mbaye hajui maana ya evidence. Tell azam tv watuonyeshe kwa ufasaha hayo matukio mawili vinginevyo shout your mouth otherwise football incidents are not avoded. maana wengine wanasema Yondani alifanya rafu mara Ngoma aliotea comeon guys don't look for excuses play football na andikeni cha maana sio hisia zenu maana mmekua hata mpira hamjui kuuusoma na muandika. Poor you Saleh

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kaka umeeleza kitu cha uhakika...saaana watuletee ushahid siyo maneno tu

      Delete
  5. Nimeangalia kwa makini goli la kwanza la Yanga ,Ngoma hakuwa off-side,aliyepawswa kuwa off-side ni Yondani lakini hakuucheza ule mpira aliupisha hivyo kuua off-side tarajiwa.Halafu Yondani hakucheza rafu alichofanya ni kutumia uzoefu kumdhibiti Miraji asiupate mpira,akili na timing ya Yondani kwenye njia ya mpira ilikuwa ya kiwango cha juu mno na ni mabeki wachache kama Shomari Kapombe,Wawa,Canavaro na Bossou ndio wangeweza kumzuia kuucheza mpira ule katika mazingira yale ambapo Miraji ndiye aliyejigonga kwa Yondani na kuanguka na kuukosa ule mpira aliodhamiria kupiga kichwa.Alichofanya Yondani ni kusimama kwenye njia ya mpira na kukaza mwili na hakumsukuma Miraji bali Miraji hakuwa na nguvu za kutosha kumuondoa Yondani kwenye njia ya mpira

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic