April 18, 2016

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), limelaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu kufanya vurugu mara baada ya mchezo kati ya Simba dhidi ya Toto Africans uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

TFF imesikitishwa na kitendo hicho cha mashabiki wa klabu ya Simba, na kusema inalaani kitendo hicho ambacho sio cha kiuana michezo, huku ikiwataka wanachama, washabiki kuheshimu viongozi wa klabu zao waliopo madarakani na kama kuna masuala ya kujadili wakayajadili katika vilabu vyao.
 Mashabiki wa klabu ya Simba walifanya vurugu kwa kurusha mawe, wakilenga kuwadhuru viongozi wa klabu hiyo pamoja na wachezaji, magari waliyokuwa nayo baada ya timu yao kupoteza mchezo dhidi ya Toto Africans kwa bao 1- 0.

Jeshi la Polisi baada ya kuwasihi mashabiki kuondoka eneo la uwanja punde tu mchezo ulipomalizika, mashabiki hao walikaidi na kuendelea kurusha mawe hali iliyopelekea jeshi kutumia mabomu ya machozi kuwatanya katika eneo hilo.

Kufutia kitendo hicho, Jeshi la Polisi lilihakikisha basi la timu ya Simba na viongozi wake wanaondoka salama uwanjani baada ya kuwatawanya mashabiki hao, kwa kupitia mlango wa karakana ya wachina waliojenga uwanja huo.

Aidha TFF imeviomba vyombo vya Usalama na Ulinzi kuwachukulia hatua kali mashabiki waliohusika na kitendo hicho, kwani kufanya vurugu ni kosa la jinai na wanapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Baadhi ya viongozi wa Simba wakiwa jukwaani wakifuatilia mchezo wa Simba na Toto.

Kocha wa Simba, Jackson Mayanja akitolewa kwenye benchi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic