May 31, 2016


Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amewataka wanaoidai klabu huyo kuvuta subira.

Hans Poppe amesema hata yeye anaidai Simba, lakini kama taasisi si rahisi kulipa madeni yote kwa mkupuo.

“Hata mimi naidai Simba na hilo liko wazi, tena tokea uongozi uliopita lakini sijasumbua kutaka kulipwa kila kitu.

“Simba ni taasisi, kila kitu kinakuwa na utaratibu na watu lazima wawe na subira,” alisema.
Hivi karibuni baada ya watu kusikia Simba imelipwa fedha za mshambuliaji Emmanuel Okwi zaidi ya 300,000 wamekuwa wakiusaka uongozi kutaka kulipwa wanachodai.


Jambo ambalo linaonekana halitakuwa rahisi kufanyika kwa kuwa Simba haiwezi kutoa fedha zote na kulipa madeni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV