May 31, 2016

MURO AKIWASALIMIA VIONGOZI WA JUU WA SIMBA WAKATI WA MSIBA HUO, RAIS EVANS AVEVA (KULIA) NA MAKAMU WAKE GEOFREY NYANGE 'KABURU'.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu kongwe ya Yanga, Jerry Muro amesema wanaoamini ana chuki na uongozi, klabu au mashabiki wa Simba, anajidanganya.

Muro amesema hayo siku moja tu baada ya kuhudhuria mazishi ya kiongozi wa zamani wa Simba, Said Pamba.

Muro alijumuika na wanachama na mashabiki wa Simba, akiwemo mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali na Rais wa sasa, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.

“Nilisisitiza hata mwanzo kuna maisha baada ya soka. Kumbuka Yanga na Simba ni watani, kwenye utani wakati mwingine kuna maneno ya maudhi.

“Sijawahi kuwa na chuki na Simba, lakini ninataka Yanga ifanikiwe kwa kuwa mimi ni Yanga hata kabla ya kuwa kiongozi. Nitabaki hivi baada ya uongozi.

“Nitaendelea kuipigania klabu yangu, hivyo kuiangusha Simba kwa maana ya kuishinda au kuichanganya ni jambo zuri kwangu.

“Lakini kusema nina chuki na mtu au watu wa Simba, utakuwa unakosea au kuwaza kitu kisicho sahihi,” alisema.


Muro amekuwa akionyesha kujiamini na kuwachanganya watu wa Simba kwa maneno yake ya kejeli ikiwa ni pamoja na kuwatunga majina ambayo yamekuwa maarufu.

1 COMMENTS:

  1. Amefanikiwa kwa kuwachanganya Simba,tuseme tu anaijua kazi yake.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV