May 13, 2016


MAHADHI (KATIKATI) AKIWA NA HUMUD (KUSHOTO) NA SABO...
Kipa namba moja wa Simba, Vincent Angbani, amemmwagia sifa mchezaji mpya wa Yanga aliyesajiliwa hivi karibuni, Juma Mahadh kwa kusema kuwa ndiye mchezaji wake bora msimu huu.

Wikiendi iliyopita Yanga ilimsajili kiungo mshambuliaji huyo kutoka Coastal Union na kumpa mkataba wa miaka miwili.


“Katika wachezaji ambao walinipa wakati mgumu msimu huu ni yule wa Coastal Union mwenye kasi sana na anacheza kwa kuhamahama nafasi (Juma Mahadh),” alisema kipa huyo alipokuwa akizungumza na gazeti hili.

AGBANI
Angban aliongeza kuwa Mahadh ndiye mchezaji pekee aliyewasumbua katika mechi za ligi kuu walizokutana na hakuna mwingine zaidi yake.


“Jamaa yule ni msumbufu na ni vigumu kumsoma haraka akiwa anakuja na mpira, kwa jinsi anavyokokota mpira hujui kama anatoa pasi, anaingia au anataka kupiga shuti, hivyo inakuwa ngumu kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kulilinda goli lako,” alisema Angbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV