May 17, 2016


Kocha wa Inter Club ya Angola, Zdravko Logarusic amewakaribisha Yanga katika ardhi ya Angola, lakini amewaonya kwamba wanapaswa kuwa makini.

Logarusic amesema kamwe haitakuwa kazi rahisi kwa Yanga kwa kuwa Waangola wanachotaka ni kusonga mbele na Esperanca ni timu ya matajiri.

“Wanachotaka Esperanca ni kusonga mbele, hivyo itakuwa ni kazi ngumu kwa Yanga. Nimesikia wana kikosi kizuri, hakika wanapaswa kupambana kweli.

“Kama mechi ingekuwa inachezwa Luanda, ingakuwa rahisi kwa Yanga. Lakini kwao Esperanca lazima kuwe na ugumu,” alisema.
LOGARUSIC
Tayari Yanga iko nchini Angola tayari kwa maandalizi ya mwsiho ya mechi hiyo ya pilik ya Kombe la Shirikisho.


Katika mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, bila ya Donald Ngoma na Thabani Kamusoko, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.

1 COMMENTS:

  1. Tuache kutishana bhana, mpira wa Angola hatutofautiani sana. Naamini Yanga wamejipanga na wanajua hilo. Haya mambo ya kutishana huwa yanawaondelea wachezaji wetu confidence!! Hata ile mechi ya Al Ahly yanga wangeshinda kama wangecheza kama walivyocheza misri, lakini yule captain wao alisema ukweli. Yanga walikosa confidence lakini walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuwatoa

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV