Ijumaa Juni 3 mwaka huu, kampuni za MultiChoice na M-Net Channels zitazindua M-Net Movies Blackout ambayo ni chaneli ya filamu mijini inayojihusisha na kutanganza mchango mkubwa wa waigizaji nyota wa filamu Wamarekani wenye asili ya Africa katika mafanikio makubwa ya tasinia ya filamu nchini Marekani, Hollywood.
Wakati nadhari kuu ya mpango huo itahusu orodha ndefu ya vipaji mashuhuri vya kimataifa vya wasanii Weusi, chaneli hii itaonyesha pia orodha ya filamu maarufu mbalimbali ambazo zitawavutia watu wa makundi mbalimbali.
Tukio hilo likienda wakati mmoja na tamasha la filamu la Wamarekani weusi (American Black Film Festiva-ABFF) ambalo ni tukio la kila mwaka lifanyikalo Miami (Florida) linaloonyesha mchango wa tasinia ya burudani inayofanywa na watu wenye asili ya Afrika kwa watazamaji duniani kote.
M-Net Movies Blackout itaonekana katika ving’amuzi vya kampuni ya DStv Premium barani kote Afrika. Jumla la filamu zaidi ya 170 zitaonyeshwa katika chaneli ya 109 kwa saa 18 kwa siku – kutoka Ijumaa tarehe 3 Juni tangu saa 12:00 asubuhi hadi saa 5:59 usiku.
Miongoni mwa mastaa ambao watajitokeza kucheza kwenye M-Net Movies Blackout ni Will Smith, Whoopi Goldberg, Kevin Hart, Tyler Perry, Wesley Snipes, Viola Davis, Morris Chestnut, Martin Lawrence, Mia Long, Vivica A. Fox na Zoe Saldana.
0 COMMENTS:
Post a Comment