Wachezaji Yanga walionekana kupandwa na hasira baada ya kumuona mwamuzi aliyewachezesha katika mechi yao dhidi ya Esperanca ya Angola.
Mwamuzi huyo na wasaidizi wake kutoka nchini Madagascar, walipanda ndege hiyo kwenye Uwanja wa Ndege wa Lucapa kwenda jiji la Luanda.
Wachezaji Yanga walionekana kukasirishwa na kuwaona, wakaanza kushauriana kuwafuata na kuwapa makavu.
Lakini viongozi wa Yanga walifanikiwa kuwazuia na kuwaambia waachane naye maana angeweza kupata sababu wakati yeye ndiye aliyeboronga.
Katika mechi hiyo, mwamuzi alionekana kwamba alipania kuimaliza Yanga ikiwa ni pamoja na kutoa kadi nyekundu kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Mbali na hivyo aliacha faulo nyingi za wazi hasa zile alizochewa mshambuliaji Donald Ngoma.
0 COMMENTS:
Post a Comment