AMODU |
Siku chache baada ya kifo cha Stephen Keshi aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taiga ya Nigeria, kocha mwingine wa timu hiyo maarufu kama Super Eagles, Shaibu Amodu naye amefariki dunia, leo.
Amodu amefariki akiwa nchini Benini, sikh tatu tu baada ya lifo cha Keshi ambaye pia alifia nchini humo.
Wakati Keshi alidaiwa kuwa na maumivu makali ya kichwa, Shaibu amefariki dunia baada ya kulalamika kuwa na maumivu makali ya kifua.
Inaelezwa baada ya kudai kifua kuzidi kuuma, aliamua kwenda kupumzika na hakuamka tena.
Amodu pia amewahi kuifundisha klabu kongwe ya Afrika Kusini ya Orlando Pirates.
Amodu pia amewahi kuifundisha klabu kongwe ya Afrika Kusini ya Orlando Pirates.
0 COMMENTS:
Post a Comment