Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm naye yuko ukumbini Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya upigaji kura.
Pluijm raia wa Uholanzi alikutana na mwenyekiti wa klabu hiyo anayemaliza muda wake, Yusuf Manji pamoja na makamu wake, Clement Sanga na kujadili mambo kadhaa.
Imekuwa ni nadra kocha huyo kuonekana na viongozi hao wa juu wa Yanga kutokana na ulivyo mfumo wa klabu hiyo kongwe nchini.
Manji na Sanga wanagombea nafasi zao kwa mara nyingine na wanaonekana wana nafasi ya kuzitwaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment