June 7, 2016


TFF na Yanga wamefanya mkutano wa pamoja na kukubaliana na uchaguzi wa Yanga uliopangwa kufanyika Juni 11.

Uchaguzi wa Juni 11 ndiyo ulikuwa unaandaliwa na Yanga ukiachana na ule ambao TFF walitaka ufanyike Juni 25, jambo ambalo Yanga hawakukubaliana nalo hata kidogo.


Kutokana na kikao hicho cha leo, Yanga sasa watafanya uchaguzi wao kama ambavyo uongozi wao ulitaka ufanyike chini ya kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo.

Blog hii, jana ilieleza namna ambavyo kikao hicho kati ya TFF kitakavyofanyika na maamuzi yatakayotoka ambayo ndiyo yaliyotoka leo.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda maarufu kama Maps amesema: "Baada ya kikao hicho ambacho upande wa TFF wawakilishi waliongoza ni Rais Jamal Malinzi na Katibu, Mwesigwa Celestine na Yanga wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deuditis, sasa Yanga wataendelea na uchaguzi wao wa Juni 11."

"Uchaguzi utasimamiwa na kamati ya uchaguzi wa Yanga, chini ya kamati ya uchaguzi ya TFF."

Kuhusiana na wale waliokuwa wamechukua fomu TFF na kusimamishwa, imeelezwa suala lao litapelekwa kamati ya nidhamu na kama wana vigezo vya kugombea watapewa nafasi ya kuendelea.

1 COMMENTS:

  1. Hapo hatuna sababu ya kuisemea vibaya Yanga,TFF ndio walichemka tangu mwanzo kwenye mchakato huu wa uchaguzi wa Yanga,TFF kwenye vitu vingi wanajichanganya mno.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic