June 11, 2016

KIMENYA (KULIA) AKIPAMBANA NA TAMBWE WAKATI HUO AKIICHEZEA SIMBA.

Ili kujiimarisha, Simba imeendelea kusaka mabeki wa kati ambao wataimarisha safu ya ulinzi.

Simba inataka kusajili beki mmoja wa kati ili kuwa msaada kwa wengine waliopo ambao ni Juuko Murshid na Novatus Lufunga.

Mabeki Salum Kimenya kutoka Prisons na Nurdin Chona, wote wawili wameapa kwamba kama dili lao likikamilika basi utakuwa mwisho wa mastraika wa Yanga, Amissi Tambwe na Donald Ngoma kuipenya ngome ya timu hiyo.

Simba inataka kuuongezea nguvu ukuta wake na Kimenya na Chona wamethibitisha kwamba, kweli wamepigiwa simu za kuweka mazingira ya kusajiliwa na timu hiyo.

Wachezaji hao walisema wapo katika mazungumzo na Simba ili waweze kusajiliwa na wana matumaini mambo yataenda sawa.

“Ni kweli Simba nazungumza nao lakini bado hatujafikia hatua ya mwisho, naamini nikisajiliwa nitajituma kuitumikia timu yangu,” alisema Chona.

Alipoulizwa kuhusu kukumbana na Ngoma na Tambwe, Chona alisema: “Nakuhakikishia nitapambana nao na nitaongeza mazoezi kwa ajili yao, naamini hawatapita kwangu.”

Naye Kimenya alisema: “Nipo katika mazungumzo na Simba, mambo yakiwa sawa nitakueleza. Kuhusu Ngoma na Tambwe binafsi nimewahi kucheza nao na kweli wapo vizuri lakini nikiwa Simba naamini hawatanisumbua, nitaongeza mazoezi binafsi kwa ajili yao.”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic