Yanga imempa nafasi ya mwisho straika wake, Hussein Javu ambaye
alikuwa kwenye mkumbo wa kutemwa na kuamua kumbakiza kwa ajili ya msimu ujao.
Javu alikuwa kwenye rundo la wachezaji zaidi ya saba ambao
wataonyeshwa mlango wa kutokea Jangwani, lakini ghafla akanusurika ikiwa ni
nafasi ya mwisho kuhakikisha anaonyesha kiwango kizuri kwenye upinzani mbele ya
Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Kpah Sherman ambaye hatima yake bado ipo
shakani.
Uhakika kutoka ndani ya kamati nyeti klabuni hapo ni kwamba Javu
amepewa nafasi ya upendeleo kuendelea kuwemo kikosini msimu ujao, huku Tegete
akipewa mkono wa kwa heri baada ya kukaa kikosini hapo zaidi ya misimu miwili
bila mafanikio.
“Javu atakuwepo, tumeamua kumpa nafasi tena ili akasaidie katika
safu ya ushambuliaji, lakini kwa Tegete hapana, tumemuacha aangalie maslahi
kwingine,” kilisema chanzo hicho.
Baadhi ya nyota wanaotajwa kutemwa ni Jerry Tegete, Rajab Zahir,
Nizar Khalfan, Alphonce Matogo, Hassan Dilunga na Hamis Thabit ambaye alikuwa
kwa mkopo Stand United.
0 COMMENTS:
Post a Comment