June 27, 2016


Siku chache baada ya Patrick Kahemele kutua ndani ya Klabu ya Simba na kukabidhiwa cho cha ukatibu mkuu, ameibuka na kuweka wazi mipango mipya kwa ajili ya kuisuka Simba ya msimu ujao.

Kahemele ambaye awali aliwahi kuwa Meneja wa Azam FC, ameeleza kufurahi kujiunga na Simba na kusema kwa pamoja atashirikiana na viongozi wenzake kuweka sawa mambo na kuifanya Simba kuwa tishio msimu ujao.

Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Kahemele alisema anatambua jinsi gani Simba imekuwa na kiu ya makombe kwa miaka minne sasa na kwamba katika utendaji wake ameahidi mapema ataanza na hilo kisha kuijenga Simba itakayokuwa na njia sahihi za kujitegemea yenyewe kujiendesha bila kuhitaji msaada kwa mtu binafsi.

“Kuna mengi ya kufanya kwa ajili ya kuiweka sawa zaidi Simba, natambua kuna hili la makombe, mashabiki wamekikosa hicho kitu kwa muda sasa, tunahitaji kikosi kikali na cha ushindani mkubwa msimu ujao pamoja na mambo mengi ikiwemo kuiweka Simba sehemu sahihi ya kujiendesha yenyewe.


“Haya yote kwa kushirikiana na uongozi naamini yatafanikiwa na Simba itakuwa kwenye mstari wake kwa mara nyingine tena, zaidi nashukuru kwanza nipo kwa mashabiki ambao watulivu, hawana tatizo na wanaelewa mambo ya soka yanavyokwenda,” alisema Kahemele.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic