July 22, 2016


Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup, shabiki maarufu wa FC Kauzu, Omary Ally ‘Chifu wa Masela’ amefunguka kuwa mashabiki wa Misosi hata wafanye nini kamwe hawataweza kufikia anga zake za ushangiliaji. 

FC Kauzu na Misosi zinatarajiwa kucheza keshokutwa Jumapili mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo kwenye Uwanja wa Chuo cha Bandari ‘Wembley’, Dar.

Chifu wa Masela amesema hatishwi na kikundi cha mashabiki wa timu hiyo kinachoongozwa na shabiki wao anayependa kuvaa pempasi kwa kuwa yeye ndiyo zaidi yao.


“Mashabiki wao siwezi kuwahofia, hata yule anayevaa pempasi kwa sababu najua hakuna anayenifikia katika kupigilia mapigo mapya katika kila mchezo, hivyo nitawashinda katika vyote, wao watulie tu,” alisema  Chifu wa Masela.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic