July 12, 2016


Uongozi wa Azam Media umesema umeamua kuongeza zawadi na kubadilisha mfumo wa utoaji ili kuongeza ushindi.

Mkurugenzi wa Azam Media, Tido Mhando amesema hayo wakati wa usainishaji wa mkataba na TFF na Bodi ya Ligi ili kuonyesha Ligi Kuu Bara kwa mara nyingine.

Tido ambaye pia ni mwandishi mwanadamizi amesema Azam Media imeendelea kujiimarisha na itaonyesha mechi za ligi kwa kiwango cha juu.

“Utoaji wa zawadi wa mfumo huu, maana yake ni kuongea ushindani. Sisi tuko tayari tumejiandaa,” alisema.

Katika mkataba uliosainiwa leo, klabu itapata Sh milioni 42 kwa mafungu matatu ambayo ni Sh milioni 126.

Fungu la mwisho la milioni 42 litatolewa kwa mfumo tofauti ambao utakuwa hivi.

Timu inayoshika nafasi ya juu katika msimamo inafaidika kwa kupata zaidi na itakwenda hivyo hadi chini.

Maana yake ligi itakapoisha, zitazokuwa juu kimsimamo zitapata fedha nyingi zaidi na zilizo chini zitaendelea kusota kwa kupata kiduchu.

Lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa kila kikosi kuona umuhimu wa kukaa juu katika msimamo wa ligi hali itakayochangia ushindani uwanjani kwa kila timu kutaka kushinda karibu kila mechi ili mwisho wa ligi ifaidike.
1 COMMENTS:

  1. Wamewashirikisha Stakeholders wote au ndio wameamua kujifungia ndani na kuwaamulia wahusika?

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV